Michezo

Rais wa Argentina amuomba Messi kutengua maamuzi ya kujiuzulu soka la kimataifa

Rais wa Argentina Mauricio Macri amemwita nyota wa soka wa nchi hiyo Lionel Messi kwa lengo la kumuomba atengue maamuzi yake ya kujiuzulu kucheza soka la kimataifa.
35B55FFD00000578-3661620-image-a-46_1467004980445

Messi alifikia maamuzi hayo baada ya timu yake kushindwa kwa mara ya pili mfululizo katika fainali za Copa America huku akiwa miongoni mwa wachezaji waliokosa mikwaju ya Penalti.

“Alimwita na kumueleza namna anavyoona fahari kwa kiwango kizuri kilichoonyeshwa na timu yake katika michuano hiyo huku akimtaka asisikilize maneno ya watu,” ilisema msemaji wa Rais Macri.

Ndani ya miaka mitatu Messi ametinga katika fainali tatu tofauti moja ikiwa ni ya kombe la dunia nchini Brazili mwaka 2014 ambapo walipoteza dhidi ya Ujerumani,na nyingine mbili za Copa America moja ikiwa mwaka 2015 na 2016 zote timu yake ikipoteza dhidi ya Chile

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents