Habari

Rais wa Brazil ahukumiwa kwenda jela

Aliyekuwa Rais wa 35 wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva amehukumiwa kifungo cha miaka tisa na gerezani kutokana na makosa matano yaliyokuwa yanamkabili kuhusiana na rushwa.

Kesi kubwa kati ya hizo ambayo ilikuwa inamkabili ni kupokea rushwa ya zaidi ya dola milioni moja za malipo ya ghorofa ya mapumziko kwa ajili ya ukarabati wake kwa kampuni ya ujenzi ya Ki Brazil, iitwayo kwa kifupi OAS.

Hata hivyo kiongozi huyo amepinga hukumu hiyo kwa madai kuwa hakuna kosa lolote alilolifanya huku mawakili wake wakijipanga kukata rufaa dhidi ya huku hiyo.

Kukumu hiyo imekuja ikiwa ni muda mfupi umepita tangu rais huyo wa zamani alipotangaza nia yake ya kugombea tena kiti cha Urais hapo mwakani . Brazil ni miongoni mwa nchi ambazo marais wake wamekuwa wakishtakiwa kwa upokeaji rushwa akiwemo rais wa sasa Michel Temer ambaye amechukuwa nafasi hiyo August 31 mwaka jana kutoka kwa mwana mama Dilma Rousseff aliyepigwa chini na Baraza la senate baada ya kumpigia kura ya kutokuwa na imani naye.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents