Habari

Rais wa EU Donald Tusk ahofia sera za Donald Trump

Rais wa Baraza la umoja wa Ulaya, Donald Franciszek Tusk amedai kuwa maamuzi yanayofanywa na Rais wa Marekani, Donald Trump ni miongoni mwa changamoto zinazoukumba umoja wao.

Katika barua ya Tusk aliyoitoa wiki hii kabla ya mkutano wa EU nchini Malta, amesema sera za Donald Trump zimeiweka EU katika hali ngumu kwa kuwa sera hizo za kigeni za Marekani zilikuwa zikifanyika miaka 70 iliyopita lakini pia ni miongoni mwa vitisho kutoka nje vinavyojumuisha China, Urusi na waislamu wenye itikadi kali kwa muungano huo.

“We cannot surrender to those who want to weaken or invalidate the Transatlantic bond, without which global order and peace cannot survive. We should remind our American friends of their own motto: United we stand, divided we fall,” imesema barua hiyo ya Tusk.

Barua hiyo ya Tusk iliongeza kuwa hawataweza kukubaliana na wale wanaotaka kudhoofisha ushirikiano wetu ambao bila amani hauwezi kufanikiwa na alimkumbusha Trump kuwa umoja ndio nguvu ya mataifa yao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents