Michezo

Rais wa Fifa ashauri kuongezwa timu kwenye kombe la dunia

Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Gianni Infantino ameshauri kuongezwa kwa timu zinazoshiriki kombe la dunia na kufikia 48 zaidi ya ahadi yake aliyoitoa wakati akiwania nafasi hiyo kuwa atafikisha timu 40.

0189420001456506358_filepicker

Ameshauli kuwa timu 16 kati ya zote zitatolewa katika hatua ya awali kabisa.

Kisha kubaki 32 zitakazoendelea katika makundi baada ya hatua ya mtoano kukamilika.

Infantino anasema kuwa mapendekezo hayo yatapelekwa katika bodi ya Fifa Januari.

”Haya ni mawazo ya kupata suluhisho la uhahika, tutayajadili mwezi huu na kufahamu nini cha kufanya mwaka 2017,” alisema Infantino mwenye miaka 46.

Infantino ambaye aliingia madarakani mwezi Februari baada ya kujiuzulu kwa Sepp Blatter.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents