Michezo

Rais wa FIFA Sepp Blatter atangaza kujiuzulu

Rais wa FIFA, Sepp Blatter ametangaza kujiuzulu wadhifa huo ikiwa ni siku chache tu baada ya kushinda uchaguzi kuongoza kwa awamu ya tano.

bb

Blatter alitangaza uamuzi huo jana.

“Nilijiskia mkamilifu kwa kugombea tena kwenye uchaguzi wa FIFA nikiamini kwamba kilikua ni kitu muhimu kwa FIFA. Uchaguzi umeisha lakini changamoto za FIFA hazijaisha,” alisema.

“Japokua nina madaraka kutoka kutoka kwa wanachamana wa FIFA, lakini sijiskii kama nina madaraka kutoka kwa dunia nzima ya wapenda soka, wachezaji na vilabu. Pia kwa watu wanaopumua na kupenda mpira na FIFA pia.

Kwa hiyo nimeamua kujiuzulu madaraka yangu niliyopewa na wanachama wa FIFA. Nitaendelea kuwa Rais hadi pale uchaguzi utakapo fanyika. Mkutano wa FIFA utakaofuatia kwenye ratiba ulitakiwa ufanyike 13 May 2016, lakini hiyo italeta ucheleweshwaji usio wa lazima. Nitaiagiza kamati iandae mkutanao mapema kadri inavyowezekana kumpata mrithi wangu.”

Blatter amestaafu akiwa na umri wa miaka 79 lakini ataendelea na majukumu yake hadi pale atakapopatikana mrithi wake.

Hatua hiyo inamweka Blatter kwenye uchunguzi pia wa tuhuma za rushwa baada ya maafisa wa juu wa shirikisho hilo kukamatwa wiki iliyopita mjini Zurich, Uswisi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents