Rais wa Gabon Bongo Ondimba ashirikiana na msanii mkongwe kuandaa albamu

Unafikiria itakuwaje endapo Rais wa nchi anapoamua kushirikiana na msanii mkubwa kutengeneza albamu ya pamoja?

Vanessa Mdee amethibitisha kuwa Rais wa Gabon, Ali Bongo Ondimba anafanya kazi ya kuandaa albamu akishirikiana na msanii mkongwe wa nchi hiyo Frederic Gassita.

Akiongea na mtangazaji wa Kings FM ya Njombe, Gami Dee amesema, “Frederic ni msanii ambaye anashirikiana sana na Rais wa Gabon Mhe. Ondimba. Yeye na Frederic wanafanya project ya pamoja inaitwa The African Queens Project, kwenye hiyo project albamu nzima ambayo itawashirikisha wasanii wa kike wa Kiafrika.”

Malkia huyo wa muziki wa Bongo Flava ameongeza kuwa wimbo wa Imara ambao ameshirikishwa na Gassitta ni ngoma ambayo itakuwa ya kwanza katika albamu hiyo inayotayarishwa.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW