Habari

Rais wa Juan Santos wa Colombia atangaza hali ya dharura

Rais wa Colombia Juan Manuel Santos ametangaza hali ya dharura ya kiuchumi na mazingira katika nchi hiyo wakati wa kipindi hii kigumu walichonacho.

Kwa sasa serikali ya nchi hiyo imepanga kukusanya dola milioni 13.9 zitakazoweza kusaidia kukabiliana na majanga ya maporomoko ya ardhi yaliyotokea mjini Mocoa kutokana na mvua kubwa iliyonyesha siku ya Jumamosi.

Mpaka sasa imedaiwa watu 262 wakiwemo na watoto takribani 44 wamefariki katika maporomoko hayo ambapo mazishi yao yamefanyika Jumatatu hii huku jitihada za kutafuta watu wengine zikiendelea.

Rais Santos ameahidi uwekezaji zaidi katika mji wa Mocoa zaidi ya ilivyokuwa awali, na kumkabidhi mamlaka waziri wa ulinzi Luis Carlos Villegas kuusimamia mji huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents