Soka saa 24!

Rais wa Malawi Joyce Banda amcharukia Madonna

Rais wa Malawi, Joyce Banda amemcharukia mwanamuziki Madonna kwa kile anachodai kudanganya kujenga shule 10 nchini humo.

David-Banda-Goes-Tour-Madonna

Joyce Banda ametoa kauli hizo wakati staa huyo akiwa ziarani nchini humo. Madonna alianzisha mradi wa Raising Malawi baada ya kuudopt mtoto wake wa kiume David Banda mwaka 2006 na mtoto wa kike Mercy James mwaka 2009 nchini humo.

Mrs Banda anadai kuwa mwanamuziki huyo hakutimiza ahadi yake ya kujenga shule ya wasichana kwa paundi milioni 10 na badala yake kuamua kujenga shule 10 bila kuwataarifu maofisa.

Alisema: “Ziko wapi hizi shule 10 alizojenga?

“Sehemu zingine alikarabati tu majengo yaliyopo tayari. Hakuna mtu anayetakiwa kuja hapa na kusema, ‘najenga madarasa bila kukaguliwa.

“Ni tusi kwa watu.”

Hata hivyo, Trevor Neilson, anayesimimia shughuli za misaada za Madonna jana alitoa maelezo ya ujenzi wa shule hizo.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW