Afya

Rais wa Mali aliyepinduliwa madarakani na Jeshi siku 10 zilizopita, alazwa hospitalini

Rais wa Mali aliyeng’olewa madarakani kupitia mapinduzi ya kijeshi Ibrahim Boubacar Keïta amelazwa katika hospitali moja mji mkuu wa Bamako, kwa mujibu wa Shirika la habari la Associated Press.

Lilinukuu vyanzo katika viwili kliniki ambako kiongozi huyo wa zamani anaripotiwa kutibiwa.

Mwanasiasa huyo wa miaka 75 alizuiliwa kwa siku kumi na wanajeshi kabla atangaze kujiuzulu na baaadae kuachiliwa huru..

Wakati wa mazungumzo ya kutafuta mwafaka wa mzozo wa kisiasa nchini Mali Bwana Keita alinukuliwa kusema kuwa hana haja ya mamlaka ya urais.

Kwa miezi kadhaa upinzani ulikuwa ukimshinikiza kujiuzulu na kumlaumu kwa kurudisha nyuma uchumi wa nchi, kudhibiti ufisadi na kushindwa kukabiliana na makundi ya kijihadi.

Chanzo BBC.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents