Habari

Rais wa Marekani Donald Trump aikanya Iran

Rais wa Marekani Donald Trump aikanya Iran

Kauli aliyoitoa rais wa Marekani Donald Trump kuhusu kulikanya taifa la Iran hasa rais wa taifa hilo bwana Hassan Rouhan imewashtua wengi.

Trump alitoa kauli hiyo kupitia ukurasa wake wa Twiter kuwa “Iran itapata madhara ambayo ni wachache sana wamewahi kukumbana nayo katika historia zao” iwapo italitishia taifa la Marekani.

Lakini kabla ya kauli hiyo ya Trump,kipindi cha nyuma rais wa Iran Bwana Hassan Rouhani awali kusema kwamba vita na Iran vitakuwa vita zaidi ya vita vingine vyote vilivyowahi kutokea”.

kauli ya Trump kupitia ukurusa wake wa Twiter

Yote yanakuja baada ya Marekani kujitoa katika mkataba wa nyuklia na Iran mwezi mei na kuanza kuiwekea Iran vikwazo juu ya utengenezaji wa Nyuklia licha ya taifa hilo la Marekani kuendelea kupingwa na mataifa kama Uingereza, Ufaransa, China, Urusi na Ujerumani wote ambao walikuwa wadau katika mkataba huo wa mwaka 2015.

Ikumbukwe kabla ya kauli hii ya Trump juzi jumapili  waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo alisema utawala wa Iran “unafanana zaidi na utawala wa Ki-mafia badala ya badala ya utawala wa Ki-serikali” waziri huyo alitoa maneno hayo wakati akiongeza na  Wamarekani wenye asili ya Iran jimbo la California.

 

By Ally Jei.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents