Habari

Rais wa Nicaragua amchagua mkewe kama mgombea mwenza

Rais wa Nicaragua Daniel Ortega amemtaja mkewe kama mgombea mwenza na makamu wa rais wakati huu ambapo anawania kuchaguliwa kwa muhula mwengine.

_90621786_beadc653-a49c-46a1-82ef-8515ed2a5252

Mkewe Rosario Murillo tayari ana wadhfa maarufu wa msemaji wa serikali na anaonekana kuwa anagawana mamlaka na mumewe.

Amekuwa akionekana katika runinga ya Nicaragua kila siku

Wakosoaji wanawashtumu wanandoa hao wawili kwa kuiendesha Nicaragua ambayo inakabiliwa na uchaguzi mkuu mwezi Novemba kama chombo chao cha kibinafsi.

Rais Ortega akiwa hazungumzi sana katika vyombo vya habari ,mkewe huonekana mara kwa mara katika runinga akijadili sera na kujikuza .

Akiwa mama wa watoto 7 wa rais huyo anajua kuongea Kiingereza na Kifaransa huku akijulikana pia kuwa mshairi.

Pia anasifa za kuvaa mavazi yenye rangi nyingi na vito vya miaka ya sitini.

Wanahabari wanasema kuwa raia wengi wa taifa hilo wanamuona bi Murillo kama mwenye uwezo mkubwa katika taifa lake kutokana na hadhi yake katika uma.

Mume na mkewe waliwasilisha makaratasi yao ya kugombea viti hivyo rasmi katika mji mkuu wa Managua wakiandamana na mshauri wakili wa chama chao cha Sandinista.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents