Habari

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari kujiteua mwenyewe kuwa waziri wa mafuta

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari Jumatano hii alitarajiwa kulitangaza baraza la mawaziri na kwamba angejiteua mwenyewe kuwa waziri wa mafuta.

maxresdefault (1)

Jumanne hii, Buhari alisema jijini New York, anakohudhuria mkutano wa mkuu wa umoja wa mataifa kuwa atajiteua mwenyewe kuongoza wizara hiyo nyeti.

Lengo lake ni kuondoa ufisadi na rushwa iliyokithiri kwenye sekta hiyo.

Rais huyo ana uzoefu kwenye wizara hiyo kwakuwa mwaka 1977, alikuwa waziri wa mafuta chini ya uongozi wa Gen Olusegun Obasanjo na alisaidia kuanzishwa kwa kampuni ya mafuta ya taifa ya Nigeria.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents