Habari

Rais wa Ufaransa ahakikisha usawa wa jinsia katika uteuzi serikali yake

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ameteua baraza la mawaziri lenye usawa wa kijinsia kuambatana na ahadi aliyoitoa wakati wa kampeni.

Rais Marcon amewateua wanawake 11 kuwa mawaziri kati ya mawaziri 22 wa bunge la ufaransa,Hata hivyo nafasi moja pekee ilienda kwa mwanamke lakini nafasi tano muhimu kwa taifa hilo alitoa kwa wanaume.

Hata hivyo Rais Macron, alisema kuwa ataanza kufanya kazi mapema na Rais wa jumuiya ya ulaya katika kubadilisha mfumo wa uongozi wake. Macron alibainisha hayo katika mkutano wake na waandishi wa habari jiji Paris.

Baraza la mawaziri wa Ufaransa:

Agnès Buzyn – Waziri wa Afya.

Bruno Le Maire – Waziri wa uchumi.

Françoise Nyssen – Waziri Wa Utamaduni.

Gérard Collomb – Waziri wa masuala ya ndani, François Bayrou – Waziri wa sheria.

Jacques Mézard – Waziri wa Kilimo na chakula.

Jean-Michel Blanquer – Waziri wa Elimu ya taifa.

Jean-Yves Le Driana – Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni.

Laura Flesseng – Waziri wa michezo.

Mounir Mahjoubi – Masuala ya dijitali.

Murielle Pénicaud – Waziri Wa Kazi.

Sylvie Goulard – Waziri mpya wa ulinzi.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents