Habari

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron aiomba msaada timu ya taifa ya Nigeria (+video)

Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amewaomba wachezaji wa timu ya taifa ya mpira wa miguu ya Nigeria (Super Eagles) na Wainejeria kwa pamoja waiunge mkono timu ya taifa ya Ufaransa kwenye michuano ya kombe la dunia.

Image result for emmanuel Macron and yemi alade
Rais Muhammadu Buhari na Emmanuel Macron

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Macron amesema kwa kuwa kwa sasa Super Eagles wametolewa kwenye michuano hiyo ni bora wangeishangilia Ufaransa ili kuwapa nguvu yakushinda kombe la Dunia.

Rais Macron amefunguka hayo yote jana Julai 04, 2018 akiwa nchini Nigeria kwenye ziara yake ya siku mbili ambapo alipitia kwenye academy ya watoto wanaojifunza mpira wa kikapu jijini Lagos.

https://youtu.be/4Kl3v9cbTqA

 

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents