Afya

Rais wa Uganda Yoweri Museveni atangaza maombi kwa ajili ya corona

Rais wa Uganda Yoweri Museveni ametangaza Jumamosi kuwa siku ya kitaifa ya maombi kwa ajili ya Covid-19.

Rais huy amesema kuwa alipata wazo kutoka kwa raia wa Ugandaambaye alikuwa na “maono kutoka kwa Mungu “.

“Mungu alikua amemuambia katika moano kwamba ninapaswa kuanda maombi, yaandaliwe kisayansi, ili Mungu atuponye na Covid-19…Ninatangaza tarehe 29 Agosti, 2020, siku ya maombi ya kitaifa na siku ya mapumziko ya umma. Kaeni majumbani mwenu au kwenye viwanja vya nyumba zenu na muombe,” Bwana Museveni alisema katika ujumbe wake wa mtandao wa kijamii.

Hadi sasa Uganda imerekodi watu 2,679 wenye maambukizi ya virusi vya coronana vifo 28.

Serikali iliweka masharti ya kudhibiti maambukizibaada ya kuthibitisha kisa cha kwanza mwezi Machi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents