Rais wa Urusi, Vladimir Putin akipongeza kikosi cha taifa hilo kupata ushindi dhidi ya Hispania

Rais wa Urusi, Vladimir Putin ameipongeza timu ya taifa hilo kwa kupata ushindi dhidi ya Hispania na kujihakikishia kusonga mbele mchezo wa michuano ya kombe la dunia inayoendelea kwenye nchi hiyo mwaka huu 2018.

Urusi ambayo ni mwenyeji wa michuano hiyo imeingia huku ikionekana kuwa timu dhaifu lakini imeweza kufanya maajabu makubwa mpaka sasa baada ya kutinga hatua ya robo fainali baada ya kuwafunga Saudi Arabia na Misri mpaka inatinga hatua ya robo fainali.

Timu hiyo ambayo imepata mafanikio makubwa mpaka sasa ya Urusi imehudhuriwa mara moja wakati wa ufunguzi na rais wa nchi hiyo wakati wa ufunguzi wa michuano hiyo ya FIFA.

Putin ameshindwa kuhudhuria kwenye mechi dhidi ya Hispania iliyopigwa kwenye dimba la Luzhniki jijini Moscow kwa sababu ya majukumu ya kiserikali yanayo mkabili.

Kwa mujibu wa msemaji wake, amesema kuwa Putin alimuita meneja wa kikosi cha Urusi, Stanislav Cherchesov kabla ya mechi na kumtakia kilalakheri na hata baada ya mchezo huo alimpa pongezi.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW