Habari

Rais wa zamani Kenya Mwai Kibaki alazwa nchini Afrika Kusini

Aliyekuwa Rais wa Kenya Mwai Kibaki, 84, amelazwa hospitalini nchini Afrika Kusini akipokea matibabu maalum baada ya kuugua mwishoni mwa wiki.

Moi-Kibaki

Kiongozi huyo wa zamani aliugua akiwa nyumbani kwake na akapelekwa hospitalini Karen, Nairobi Jumamosi jioni kabla ya kusafirishwa Afrika Kusini Jumapili.

“Aliandamana na daktari wake. Tunamtarajia arejee nyumbani hivi karibuni, na Wakenya watafahamishwa kuhusu hali yake wakati mwafaka,” taarifa iliyotolewa na familia yake ilisema.

Desemba mwaka 2002, Bw Kibaki aliumia baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani wakati wa kampeni na akapelekwa Uingereza kwa matibabu.

Aliapishwa kuwa rais muhula wake wa kwanza akiwa kwenye kiti cha magurudumu.

Mkewe, Lucy Muthoni Kibaki, alifariki Aprili mwaka huu akitibiwa jijini London.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents