Habari

Sad: Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela afariki dunia

Rais wa zamani wa Afrika Kuisni Nelson Mandela, amefariki dunia huko Johannesburg, Afrika Kusini usiku wa jana Alhamisi (December 5) akiwa na umri wa miaka 95.

Mandela2

Mandela alikuwa anatibiwa homa ya mapafu nyumbani kwake baada ya kulazwa hospitalini kwa miezi mitatu.

Katika taarifa yake kwa watu wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, alisema kuwa Mandela amewaaga lakini yuko mahali salama.

Rais Zuma amesema kuwa taifa limepoteza mtu waliyemjua kama mtoto wa taifa hilo.

Mandela aliwahi kushinda tuzo ya amani ya Nobel, na kutambulika kama rais aliyeheshimika sana hasa kwa kupatanisha watu wa Afrika Kusini baada ya kuondoka gerezani.

Pumzika kwa amani Nelson Mandela

CHANZO: CNN/BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents