Habari

Rais wa zamani wa Brazil apandishwa mahakamani

By  | 

Aliyekuwa Rais wa Brazil, Luiz Inacio Lula da Silva ametoa ushahidi wake Jumatano hii mbele ya Jaji wa mahakama nchini humo, anayeshughulika na masuala ya kupambana na rushwa katika moja ya kesi zinazomkabili kiongozi huyo kati ya tano anazotuhumiwa.

Jaji alisikiliza kesi hiyo kwa takribani saa tano huku maelfu ya watu wanaomuunga mkono rais Lula wakiwa nje ya mahakama hiyo.


Maelfu ya watu wanaomuunga mkono Rais Luiz Inacio wakimsindikiza mahakamani

Kosa jingine analoshtakiwa Lula ni kupokea nyumba ya kifahari kama hongo katika kashfa ya rushwa inayohusisha kampuni ya mafuta ya taifa ya nchi hiyo, Petrobras.

Jopo la mawakili anayesimamia kesi ya kiongozi huyo, Valeska Zanin amesema kuwa kesi hiyo inamsukosuko wa kisiasa ndani yake na hivyo mteja wao hana hatia yoyote.

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments