Michezo

Rais wa zamani wa FIFA Joao Havelange afariki dunia

Rais wa zamani wa FIFA Joao Havelange amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 100. Mbrazil huyo alikuwa mtangulizi wa Sepp Blatter katika shirikisho la mpira wa miguu duniani kuanzia mwaka 1974 hadi 1998.

joao-havelange-750px_0

Taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari vya Brazil viliripoti kuwa Havelange amefariki asubuhi ya Jumanne kwa saa za Brazil. Andresa Feijo ambaye ni msemaji wa hospitali aliyokuwa amelazwa Havelange, alithibitisha kutokea kwa kifo cha gwiji huyu. Aliweka wazi pia kuwa amekuwa akitibiwa Pneumonia tangu mwezi Julai.

Mwaka 2013, Havelange alijiondoa kuwa Rais wa heshima wa shirikisho la soka duniani FIFA, baada ya kusemekana kuwa alipokea hongo/rushwa.

Alikuwa mmoja wa wanakamati wa Olympic (IOC), kuanzia mwaka 1963 hadi 2011 alipojiuzulu kwa sababu ya kudhoofu kwa afya yake.
Havelange aliiwakilisha Brazil katika mashindano ya Olympic ya Kuogelea mwaka 1936,mwaka ambao aliidhinishwa kuwa mwanasheria kabla ya kuchaguliwa na IOC.

Akiwa kiongozi wa FIFA aliongeza washiriki wa kombe la dunia kutoka timu 16 hadi 32, ambapo mashindano 6 yalifanyika chini ya utawala wake.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents