Habari

Rais wa zamani wa Korea Kusini Park Geun-hye ahukumiwa miaka 24 jela na faini ya bil 38

Mahakama ya Korea Kusini imempata na hatia Rais wa zamani wa nchi hiyo, Park Geun-hye.

Geun amekutwa na makosa 18 ikiwemo kutumia vibaya madaraka yake na kupokea rushwa hivyo mahakama hiyo imemuhukumu kifungo cha miaka 24 gerezani.

Akisoma hukumu hiyo Jaji wa Mahakama hiyo alisema, “The President abused the power which was given to her by the citizens.” Hakimu huyo aliongeza kuwa hukumu kali ilihitajika ili kutuma ujumbe wa wazi kwa viongozi wa baadaye wa nchi hiyo.


          Wafuasi wa Park Geun-hye wakiwa nje ya mahakama

Hata hivyo waendesha mashitaka walimwomba Hakimu kumhukumu Geun kifungo cha miaka 30 jela. Pia Rais huyo wa zamani wa Korea Kusini atatakiwa kulipa faini ya dola milioni 17 mbazo ni zaidi ya shilingi bilioni 38 za Kitanzania.

Kesi ya Geun a=ilifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanaza January 3 mwaka jana japo kiongozi huyo hakuweza kuhudhuria mahakamani hapo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents