Habari

Rais wa zamani wa Marekani, Bush aahidi kumpigia kura Hillary Clinton

Rais wa zamani wa Marekani kupitia chama cha Republican, George HW Bush amedai kuwa atampigia kura mgombea urais wa chama cha Democratic, Hillary Clinton kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Novemba, mwaka huu.

3600

HW Bush ambaye ni baba mzazi wa rais aliyemuachia madaraka Obama, George W Bush anadaiwa kutoa kauli hiyo na kumwambia Bi. Kathleen Kennedy Townsend ambaye alikuwa ni Gavana wa mji wa Maryland lakini pia ni mpwa wa rais wa zamani wa nchi hiyo John Kennedy aliyeuawa mwaka 1963.

Bi. Kathleen ameweka picha kwenye mtandao wake wa Facebook akiwa na rais huyo mstaafu na kuandika ujumbe unaosomeka, “The President told me he is voting for Hillary!!.”

640
Picha aliyoiweka Bi. Kathleen kwenye mtandao wake wa Facebook

Bush alikuwa rais wa 41 kuiongoza nchi ya Marekani kuanzia mwaka 1989 – 1993.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents