Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Rais wa zamani wa Marekani George Bush ampigia magoti Heather Lind

Aliyekuwa rais wa 41 wa Marekani, George Herbert Walker Bush amemuomba msamaha muigizaji wa kike wan chi hiyo Heather Lind kwa kosa la kumnyanyasa kijinsia.

Lind kupitia mtandao wake wa Instagram, aliandika ujumbe wa kumtuhumu rais huyo wa zamani kwa kosa la kumfanyia unyanyasaji huo mwaka 2014 wakati wakijiandaa kupiga picha ya pamoja kwenye siku ya sherehe za Mapinduzi ya Vita ya Marekani mjini Washington.

Hata hivyo muigizaji huyo aliufuta ujumbe huo muda mfupi baada ya kuutuma kwenye mtandao huo.

Wakati huo huo kupitia kwa msemaji wa Rais Bush amesema, kiongoziu huyo wa zamani wa Marekani alisema kuwa alifanya katika hali ya ucheshi lakini anaomba msamaha kwa muigizaji huyo kama kitendo hicho kilimkwaza.

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW