Tupo Nawe

Rais wa zamani wa Tunisia, Zine el-Abidine Ben Ali aaga dunia

Rais wa zamani wa Tunisia Zine el-Abidine Ben Ali amefariki dunia akiwa uhamishoni, familia yake imesema.

Image result for zine el-abidine ben ali

Kwa mujibu wa shirika la habari la VOA, Ben Ali aliiongoza nchi hiyo kwa miaka 23 na alikuwa amesifika kwa kuleta utulivu na neema ya kiuchumi. Lakini alikosolewa na wengi kwa kukandamiza uhuru wa kisiasa na vitendo vya ufisadi vilivyokuwa vimekithiri.

Mwaka 2011, alilazimishwa kuachia madaraka baada ya maandamano makubwa yaliyojiri mitani. Hili lilisababisha wimbi la maandamano kote katika maeneo ya Kiarabu yaliyokuwa yakijulikana kama Arab Spring.

Nchi nyingi zilijikuta marais wao wakiondoka madarakani ama kuzuka kwa migogoro baada ya kiongozi huyo wa Tunisia kulazimishwa kuachia madaraka, na harakati hizo kupewa jina la Arab Spring.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW