Burudani

Rama D aja na suluhisho la kuwafanya madj wa club kucheza Bongo Flava kuliko muziki wa Naija

Muimbaji wa R&B, Rama Dee ambaye kwa sasa makazi yake yamehamia nchini Australia, ametoa maoni yake kuhusiana na mabadiliko aliyoyaona katika sehemu mbalimbali za burudani nchini.

RAMA_DEE___

Msanii huyo ambaye amekuja kusalimia nchini, alikuwa akiongea kwenye kipindi cha E-News cha EATV na kudai kuwa kama wasanii wa Tanzania watafanya muziki wa Kitanzania, muziki wao utachezwa zaidi kwenye club kuliko muziki wa kigeni.

“Unajua tokea nimekuja hapa Bongo kila sehemu ninayoenda club na sehemu zingine za burudani, naona madj wanapiga sana nyimbo za Kiafrika, kitu kizuri pia na kibaya maana uzuri wanathamini muziki wa Afrika na ubaya naona wanapiga sana nyimbo za Nigeria kuliko za kibongo,” alisema.

“Lakini bado wasanii wa Bongo wana uwezo wakufanya juhudi zaidi kwa kufanya kazi nzuri ili nyimbo zichezwe zaidi. Cha muhimu wanatakiwa kufanya kitu cha Kitanzania zaidi ili kuleta ushindani kati ya wanigeria na sisi.”

Related Articles

Leave a Reply

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents