Rama Dee afanya video ya kimataifa nchini Australia


Kimya kingi kina mshindo mkuu. Baada ya kukaa kimya kwa muda, msanii anayeheshimika zaidi katika muziki wa R&B nchini, Rama Dee, amesema mashabiki wake wa muziki wakae mkao wa kula kupokea video ya kimataifa aliyoifanya nchini Australia.

“Huu ndio muonekano wa video mpya ya Rama Dee baada ya “Kuwa Na subira” kazi imefanyikia Australia Gold cost,Kiwango ni kizuri cha kimataifa so kaa sawa unajua ni ngoma gani!!??…tega macho na mackio pia nashukuru sana kwa kuweza kuupokea vizuri mziki mzuri unaofanywa na mimi,,,pa1 sana,” ameandika leo kupitia Facebook.

Rama Dee akiwa na mwanae
Kwa sasa Rama Dee anaishi huko Brisbane, Queensland, Australia ambako ameoa raia wa nchi hiyo na wana mtoto mmoja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents