Burudani

Rama Dee: Kuachia Sio waoaji hao videoni.

Msanii mkongwe wa r&b Rama D. Anatarajia kuachia ngoma mpya kabisa kwenye audio na video moja kwa moja.
Akizungumza na bongo5 Rama D alisema anatarajia kuachiachia hayo mating’a wiki hii “katikati ya wiki hii natarajia kureliz nyimbo yangu mpya inayoitwa Sio waoaji hao kwenye oudio na video kwa pamoja”

 

Akielezea ngoma yake hiyo mpya Rama D alisema hii video imefanywa na mtayarishaji mkali Jasmine kutoka nchini australia huku ngoma yenyewe ikiwa imefanywa katika studio za sababisha record.

Pia Rama D alisema baada ya kuachia ngoma hiyo pia hatochelewa kuachia ngoma nyingine aliyeitaja kwa jini la make up ambayo imefanyika katika studio za B Hits huku ukiwa ni mkono produza mkali Pancho Latino “baada ya kuachia ngoma yangu ya sio waoaji hao sintkaa kwa muda mrefu kwani kuna ngoma ambayo nitaiachia mapema tu ikiwa ni kama baada ya wiki mbili au tatu hivi inaitwa make up niliyoifanya kwa Pancho Latino pale B Hits”
Aki zungumzia ukimya wake wa muda mrefu msanii Rama D alisema kua alikuwa kimya kwa muda mrefu kutokana na kuwa na show nyngi nje ya nchi na ndi kitu kilichomfanya achelewe kumalizia video yake ya make up ila aliwaambia mashabiki wake wakae tayari tu kwani anaimani watfdurahia ngoma zangu “mashabiki wangu wakae tayari kwani ninaamini watafurahi vya kutosha kwani nimejikoki na nina madini ya kutosha kabisa”

Kwa upande mwingine ameweza kuwashukuru mashabiki kwa kuwaambia “nawashukuru sana mashabiki wanaojua nini maana ya r&b na wanaelewa mziki mzuri upo wapi hivyo ndio maana wananipa sapoti ya kutosha hivyo natumai sinto waangusha na wategemee kufurhia muziki mzuri kutoka kwangu”.
Kwa sasa Rama D yupo chini ya studio za sababisha huku akiwa chini ya usimamizi wa mtu mzima Jors Bless.
Kila la kheri kaka

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents