Michezo

Ramires kujiunga na klabu ya Jiangsu Suning ya China

Kiungo wa kimataifa wa Brazil na klabu ya soka Chelsea Ramires Santos do Nascimento anategemea kujiunga na timu ya Jiangsu Suning ya China.

Pg-73s-pele-getty

Kiungo huyo mwenye miaka 28 Chelsea ilimsajili toka Benfica, mwaka 2010 kwa pauni milion 17 na inatarajiwa timu hiyo inayocheza ligi kuu ya china iko tayari kutoa dau la pauni million 25 kumnasa nyota huyo.

Ramires, alisaini mkataba mpya wa miaka minne mwezi Octoba,mwaka jana, lakini msimu huu ameanza kikosi cha kwanza kwenye michezo saba tu ya ligi ya England.

Timu ya Jiangsu ilimaliza katika nafasi ya nane kwenye msimu wa mwaka 2015, na kikosi hicho kinanolewa na nyota wa zamani wa Chelsea Dan Petrescu.

Kiungo huyu wa kibrazil akiwa na The Blues, ametwaa ubingwa wa ligi, kombe la Fa,kombe la ligi , ubingwa wa klabu bingwa ulaya na ile michuano ya Europa ligi

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents