Aisee DSTV!

Ramos agusia hatma yeke baada ya miaka 14, Rais wa Madrid ashtuka, United na PSG zamtolea macho

Sergio Ramos huwenda akaondoka ndani ya klabu ya Real Madrid kipindi hiki cha majira ya joto baada ya kuitumikia kwa miaka 14, kwa mujibu wa vyanzo mbali mbali vya habari kutoka nchini Hispania.

Real Madrid star Sergio Ramos has shocked the club by admitting he may leave this summer

Mitandao ya ‘El Chiringuito’ na Marca imeripoti kuwa nahodha huyo huwenda akaondoka ndani ya Bernabeu muda wowote.

Ramos amekosa jumla ya mechi saba za msimu siku za hivi karibuni kwa kile kinachodaiwa kusumbuliwa na majeraha na kutarajiwa kurejea Hispania mwezi Juni.

Hata hivyo nyota huyo amekuwa na msimu mbaya huku akikumbana na kifungo mwezi Machi kwenye mechi yao dhidi ya Ajax.

Real are desperate to move players on but Ramos is not one Zinedine Zidane wants to lose

Huku akiwaudhi mashabiki baada ya kuachia kipande chake cha video ambacho kinaonyesha maisha yake ya soka wakati ambao timu yake inapata kichapo cha mabao 4-1.

Kutokana na vyanzo vya habari kutoka nchini Hispania vinaeleza kutokuwepo na mahusiano mazuri baina ya klabu na mchezaji huyo kwakuwa, Ramos hana furaha kwa kitendo cha rais wa timu hiyo, Florentino Perez kuwakoromea wachezaji kwenye vyumba vya kubadilishia nguo baada ya kupoteza mchezo.

Madrid inayotabia ya kuwasumbua wachezaji lakini sio kwa Ramos ambaye bado anahitajika na kocha wa timu hiyo,  Zidane na kamwe hawezi kukubali kumpoteza.

Kama klabu italazimika kuangalia swala hilo kwa upande mwingine hasa kutokana na timu kadhaa kuja na ofa kubwa ambazo zinalenga kumng’oa nyota huyo ikihusishwa na Manchester United ambayo Ramos alitamani kujiunga nayo tangu mwaka 2015.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW