Mitindo

Rangi ya mwaka 2017, ‘Greenery’ inavyobamba

Kampuni ya rangi Pantone imesema kuwa, kwa kipindi cha mwaka wa 2017, rangi ijulikanayo kama Greenery ndio inayonoga.

Rangi hiyo yenye asili ya kijani itatumika zaidi kwa kipindi hiki katika nyanja mbalimbali ikiwemo mitindo na majumbani.


Kuashiria rangi ya Greenery imeanza kukubalika, tayari baadhi ya wabunifu wameanza kuitumia rangi hiyo katika maonesho ya mavazi, kama ‘Women’s Spring Fashion 2017’ na imeonekana kupokelewa vizuri.

Mastaa kibao wameshaanza kuonekana wakitumia Greenery kwenye mitoko yao. Miongoni mwao ni Lupita Nyong’o,Tilda Swinton, Rita Ora na wengineo.

Tazama video fupi, jinsi ambavyo Pantone walizindua rangi hiyo.

Na Laila Sued.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents