Jiunge ufaidi miezi 2 bure!

Rapa Craig Mack aliyewahi kuvuma duniani na wimbo wa ‘Flava In Ya Ear’ afariki dunia

Rapa mkongwe nchini Marekani, Craig Mack ambaye ni moja ya wasanii wa kwanza kusainiwa kwenye lebo ya Bad Boy Records amefariki dunia usiku wa kuamkia leo Machi 13, 2018  nyumbani kwake Walterboro mjini Carolina kwa ugonjwa wa shambulio la moyo.

Craig Mack

Craig (46) miaka ya 90’s alitamba na wimbo wa ‘Flava in Ya Ear’ na kujizolea umaarufu duniani na kuchukua tuzo kibao kupitia Remix ya wimbo huo ambapo alimshirikisha Notorious B.I.G .

Taarifa za msiba huo zimesambaa kufuatia watu maarufu nchini humo wakiwemo Ma’DJ wa vituo vya radio kutoa salamu za rambi rambi.

Baada ya kutemana na lebo ya Bad Boy Records, Craig alijiunga na lebo ya Scotti Brothers Records mwaka 1997 ambapo alifanikiwa kuachia albumu moja ya Operation: Get Down .

Hata hivyo, mpaka mauti yanamkuta Craig alikuwa ni muumini mzuri wa dini na alikuwa ameshajiweka kando na muziki wa kidunia.Tazama video ya wimbo wa ‘Flava in Ya Ear’ remix

 

 

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW