DStv Inogilee!

Rapa Rosa Ree, Moozle, Gigy Lamayne na Rouge waungana kufanya remix ya wimbo wa U.N.I.T.Y wa Queen Latifah (+audio)

Leo Machi 8, 2019 ni siku ya wanawake duniani na siku hii ni muhimu kuangalia changamoto na mazuri yaliyofanywa na wanawake kwenye jamii, na hii imejidhihirisha kwa wasanii wa kike wa muziki wa Hip-Hop barani Afrika Rosa Ree (Tanzania), Rouge, Moozlie na Gigy Lamayne wote kutoka Afrika Kusini na Mz Kizz kutoka Nigeria. Ambapo wasanii wameurudia wimbo wa Malkia wa Hip Hop duniani Queen Latifah.

Usikilize wimbo hapo juu

Lengo la kufanya remix hiyo ni kuonyesha nguvu pale wanawake wanaposimama pamoja na kuimarisha umoja kupitia muziki.

Ngoma hiyo ambayo imefanyika Afrika Kusini, ina ladha ya lugha tofauti tofauti ikiwemo kiswahili na kizulu.


Kwenye mahojiano yake na waandaaji wa wimbo huo ambao ni Castle Lite, Rosa Ree amesema “wimbo mwingine unaoshirikisha wasanii wa kike wa Hip-Hop, ni wimbo wa kusherehekea mazuri ya wanawake waliotangulia kwenye muziki, na sio tu kwa wanawake wa Afrika bali katika kila sehemu ya dunia, kuweka uhai katika nguvu ya mwanawake katika muungano.”.

Akizungumza baada ya onyesho hilo, Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Silke Bucker amesema “Msingi wetu kama Castle Lite kila siku umekuwa ni kuvuka mipaka kwa kutumia ubunifu, na ili kuweka kumbukumbu katika siku hii ya kipekee ya Wanawake, hakukuwa na njia nzuri zaidi kwetu kuunganisha wanawake zaidi ya muziki,”

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW