Burudani

Rapa wa Kenya ala shavu kwenye filamu ya Hollywood

By  | 

Msanii wa Kenya anayeishi nchini Norway, Stella Mwangi amepata shavu la wimbo wake kusikika kwenye filamu ya mjini Hollywood, Marekani.

Wimbo wake wa ‘Big Girl’ umesikika kama soundtrack katika filamu ya “Rough Night” ambayo itaanza kuonekana Juni 16 mwaka huu.

Kupitia mtandao wa Instagram, rapper huyo wa kike amendika, “? I’m excited to confirm that ‘Big Girl’ off my latest Hollywood EP Album #StellaMwangi is trailer soundtrack to Hollywood movie #RoughNightMovie.” Sinema hiyo ina nguli wa uigizaji kama Scarlett Johanssen.

Hata hivyo Stella ameonekana kumzimia zaidi Vanessa Mdee baada ya kumuandikia ujumbe Jumatano hii katika Woman Crush Wednesday (WCW) kwa kumuandikia ujumbe muimbaji huyo wa Bongo Fleva kupitia mtandao wa Twitter.

“My #WCW today is the pop queen herself @VanessaMdee. Hit after hit, Vee Money be the major?. Slay girl!,” ameandika Mwangi katika mtandao huo.

Loading...

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Comments