Burudani

Rapa wa Marekani MIMS ndiye aliyetoa jina la kundi ‘Bongolos’ – P Funk

Prodyuza mkongwe kutoka Bongo Records, P-Funk Majani ambaye hivi karibuni alitambulisha rasmi kundi lake jipya la Bongolos, amesema jina la kundi hilo lilitolewa na mkali wa ‘This is Why Im Hot’, MIMS.

P-Funk amesema kuwa wazo hilo lilipatikana kupitia wimbo wa ‘You Can Never Be Me’ alioutayarisha yeye ambapo Jay Mo alisikika sambamba na MIMS, miaka mitano iliyopita.

“Tangu tulivyopiga ile ngoma na tukapata vocal za MIMS na Jay Mo akaweka vocal na jamaa mwingine wa Marekani anaitwa Immu Cabir, kwenye verse ya MIMS alichana akasema ‘Welcome to the Jungle, Bongolos… yaani nikasema hili ni jina la kundi, Bongo Records, Bongo Flava,” P- Funk aliiambia Friday Night Live ya East Africa TV.

Alifafanua kuwa maana ya jina hilo ni Uafrika na utafutaji wa watu ambao ni kama wanaishi msituni.

Bongolos inayoundwa na wasanii wawili akiwemo msanii wa kike ‘Tamu’, wameachia wimbo wao wa kwanza waliouita jina la ‘Wape’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents