Burudani

Rapper DMX akamatwa kwa kukwepa kulipa kodi

Rapper kutoka nchini Marekani anayeunda kundi la Ruff Ryders, DMX akamatwa na polisi kwa makosa 14 ya ukwepaji kodi na rushwa.

Kwa mujibu wa CBS rapper huyo anadaiwa kiasi cha dola milioni 1.7, inadaiwa kuwa msanii alifungua akaunti ya benki nyingine na kutumia jina jingine ili kukwepa kodi.

“For years, Earl Simmons, the recording artist and performer known as DMX, made millions from his chart-topping songs, concert performances and television shows. But while raking in millions from his songs, including his 2003 hit ‘X Gon’ Give it to Ya,’ DMX didn’t give any of it to the IRS.” wamesema wanaohusika na kodi IRS ( Internal Revenue Service).

Imeripotiwa kuwa DMX ameingiza zaidi ya dola milioni 2.3 kwa mwaka 2010 hadi 2015 lakini msanii huyo alikwepa kulipa kodi. Endapo akikutwa na hatia kutokana na makosa aliyonayo basi miaka 44 atatumikia jela.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents