Habari

Rapper Fat Joe ahukumiwa kifungo cha miezi 4 jela kwa kushindwa kulipa madeni ya kodi!

Inavyoonekana mdudu ‘madeni’ anawasumbua mastaa wengi hususani wanamuziki wakubwa ambao wengi wao hukabiliwa na madeni ya kodi kitu kinachoashiria pia kushuka kwao kiuchumi.

Fat-Joe

Rapper Joseph Cartagena maarufu kama Fat Joe (June 24) amehukumiwa kifungo cha miezi minne nyuma ya nondo (jela) baada ya kushindwa kulipa madeni la kodi (income taxes) ya zaidi ya $1 MILLION kwa miaka miwili.

Kwa mujibu wa TMZ mwaka jana mwishoni Joe mwenye miaka 42 alikili kukwepa kuilipa serikali kodi na kuahidi kuwa atachukua jukumu la kulipa madeni hayo.

Kifungo hicho cha miezi minne jela kitaambatana na faini ya $15,000 pamoja na usimamizi maalum wa mwaka mmoja baada ya kutoka jela.

Fat Joe anatakiwa kuripoti jela (August 26) kuanza kutumikia kifungo chake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents