Burudani

Rapper King Kaka afunguka kuhusu ‘Life na Adabu’

King Kaka amefunguka sababu ya kuachia wimbo wake mpya ‘Life na Adabu’.

Rapper huyo ambaye ameachia wimbo huo kwa ajili ya kuwahamasisha vijana, ameiambia Bongo5, “Nina furaha kwamba ninaweza kuburudisha na wakati huo huo nahamasisha na kufundisha kizazi. Wao ni watu wangu na mimi natakiwa kuwaangalia.”

“Ni bahati ninaweza kutumia muziki wangu kuwahamasisha na kufika mbali. Kama mwisho wa siku muziki wangu utaathiri mtu au kuwasaidia kwa njia fulani nitakuwa nimefikia malengo yangu,” ameongeza.

Wimbo huo umetayarishwa na Ricco Beats huku Mix na Master ikifanywa na Richie G, na video imeongozwa na Tahi kutoka Tattuah Films. Tazama video hiyo hapa chini.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents