Burudani

Rapper Kush Tracey akana kuwa mtumiaji mkubwa wa vileo

Msanii wa muziki Kush Tracey ni miongoni mwa rappers wa kike wanaofanya vizuri nchini Kenya.

Anafahamika kama ‘bad girl’ kwenye game na walimake headlines mwaka jana yeye pamoja na Timmy Tdat walipotengana baada ya kuwa wapenzi kwa muda mchache mno. Kupitia kipindi maarufu cha burudani nchini Kenya Mambo Mseto, Mzazi Willy Tuva alimkalisha chini wakapiga stori kuhusu jinsi maisha yake yanavyoenda hususan baada ya kutengana na aliyekuwa mpenzi wake Timmy Tdat.

Tuva alitumia fursa hiyo kumwuliza pia na issue nyingine ambazo zimekuwa zikimzunguka na wakati huu aliulizwa kuhusu uhusiano uliopo kati yake na chupa. Alianza kwa kukubali kwamba ni mtumiaji ndio…”Occasionally but sio kuoverdo I maintain bana, sio ile ya kuharibu, kidogo tu unajua ile hype, unapata kidogo na ile tu ya kwa starehe tu, unatulia tu. Nilianza kunywa nikiwa Campus ile influence, but am glad sijawahi kupotelea hapo. Like it’s not a priority like ile kitu ya once in a while. Sio kila siku tu,” alisema Kush Tracey.

Kuhusu ex wake, aligoma kuelezea iwapo anammiss au vingine. “No am good, am good. Yaliyopita si ndwele tugange yajayo, but the working relationship was good.”

Na: Teddyza Agwa
Instagram @teddybway

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents