Burudani

Rapper mdogo zaidi apata dili Atlantic Records

Rapper mdogo wa kike Danielle Bregoli maarufu kama Bhad Bhabie amesaini mkataba na lebo kubwa ya muziki duniani, Atlantic Records.

Kwa mujibu wa mtandao wa TMZ, msanii huyo ambaye ana umri wa miaka 14 ametajwa kuingiza fedha nyingi zaidi kupitia mkataba huo aliosaini na Atlantic.

Bhad Bhabie yupo kwenye chati za Billboard Hot 100 ambapo wimbo wake mpya ‘These Heaux’ aliouachia mwezi August mwaka huu ambao pia umetazamwa zaidi ya mara milioni 22 YouTube unashika nafasi ya 77.

Msanii huyo anaungana na mastaa wengine kwenye lebo hiyo akiwemo Bruno Mars, Ed Sheeran, Wiz Khalifa na Cardi B

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents