Tupo Nawe

Rapper Nipsey Hussle aagwa kifalme, Obama aungana na waombolezaji, shuhudia tukio lilivyokuwa (+ Video)

Wengi wakimjua kama Nipsey Hussle lakini jina lake la kuzaliwa likiwa ni Ermias Joseph Asghedom aliyezaliwa miaka 33 iliyopita August 15, 1985 kusini mwa Los Angeles nchini Marekani na kupoteza maisha yake March 31, 2019 (age 33) Los Angeles, California, U.S.A ikiwa ni nje ya duka lake la nguo. ambalo linaitwa ‘The Marathon Clothing”

Usiku wa kuamkia leo ndio ilikuwa siku maalumu ya kumuaga rapper Nipsey ambaye alipigwa risasi nje ya duka lake March 31, 2019. katika siku hiyo ya kumuaga Nipsey mastaa wengi sana walihudhuria katika ukumbi huo ambao ndio ilikuwa sehemu alipoagiwa Michael Jackson ukumbi wa Stemple Center Los Angeles California nchini Marekani.

Msanii @jheneaiko Amepata Nafasi ya Kutumbuiza Katika Ibada ya Mwisho ya Kutoa Heshima Kwa Rapper #NipseyHussle

Wimbo Huu Unaitwa #EternalSunshinena Ame-Perfome #JheneAiko Mbele ya Umati wa Watu waliohudhuria Katika Sherehee Hizi za Mwisho kwa Nipsey

#LaurenLondon Ambae Alikua Mpenzi wa #NipseyHussle Akitoa Neno lake la Mwisho Katika Ibada ya Mwisho ya Kutoa Heshima Kwa Nip Huku Akionesha Ujasiri Kwa Kutangaza Kuwa Movement Alizokuwa Akifanya Mpenzi wake Zitaendelea #TheMarathonContinues

Lakini Pia Amezungumzia Jinsi Gani Alimpenda #NipseyHussle na Bado yupo Moyoni Mwake na Anajivunia Kuwa na Mtu Kama Yeye Maishani Mwake na Anamuombea Mpaka Watakapokutana tena
Rapper @snoopdoggAkimuelezea #NipseyHussle Kwa Jinsi Alivyomfahamu na Jinsi Alivyokuwa na Akili Katika Upande wa Biashara ya Muziki na Yeye ni Mfano mzuri wa watu walioshauriwa na Nip Utafikiri alikua Kwenyw Industry kwa Zaidi ya Miaka 15 Nyuma
Rais Mstaafu wa Marekani @barackobama Ametuma Barua Maalum Ambayo Imesomwa na #KarenCivil Akitoa Pole kwa Familia, Marafiki na Watu wote waluoguswa na Kifo cha Rapper #NipseyHussle

Katika Sehemu ya Barua Hiyo ya #BarackObama Ameeleza Kuwa, Hakuwahi Kuwa na Ukaribu na Nip lakini Watoto wake walikua Mashabiki zaidi wa Kazi zake na Aliona Nguvu ya Mchango wake kwenye Jamii Katika Kipindi chake cha Uongozi .


#StevieWonder
 ni Moja Kati ya Msanii Ambae Amepata Nafasi ya Kuimba Kwenye Shughuli za Kuaga Mwili wa Rapper #NipseyHussle

Sherehe Hizi za Kutoa Heshima za Mwisho na Kumuaga #NipseyHussleZinafanyika Katika Ukumbi wa Staples Center Huko Los Angels Marekani

Huyu ni #KameronCarterambae 
@laurenlondon alimpata Kutoka Kwa @liltunechi na Hivi ndio Jinsi alivyokua akitoa heshima zake za mwisho kwa #NipseyHussle ambae alikuwa ni Baba yake wa kambo
Kaka wa Marehemu #NipseyHussle anayeitwa #SamielAsghedom Akizungumzia Jinsi Mdogo wake Alivyokua Anaishi nae Tangu Utotoni na Walikua Katika Maisha ya Furaha na Utani Sana
Baada ya Watu mbalimbali Kutoa heshima Zao za Mwisho Wazazi wa #NipseyHussle Wametoa maneno yao ya mwisho kwa Mtoto wao Nipsey.

Mama yake Nipsey alezea maisha ya Nipsey na jinsi alivyoishi na watu Vizuri na Alivyokua anajitahidi Kushirikiana Katika Kila Aina ya Shida na Raha
Baada ya Kumaliza Kutoa Heshima zao za Mwisho Kwa #NipseyHussle , Mastaa Mbalimbali, Marafiki Na Ndugu Wakitoka Katika Ukumbi wa Staples Center

#Diddy #Usher ni Mojawapo wa Watu hao Na Wameonekana Katika Video Hii Wakiingia Kwenye Magari Yao na Kuondoka Eneo la Tukio
Hivi Ndio Ilivyokua Katika Upande wa Nje wa Ukumbi wa Staples Center ambapo Mwili wa #NipseyHussle Ulikua Umefika Kwa Ajili ya Ibada ya Mwis
Familia ya #NipseyHussleWalivyokua Mbele Kwa Ajili ya kusema Kitu Kwa Mpendwa wao Kwenye Ukumbi wa Staples Center na Sehemu Hii ya Video Imewagusa sana Watu Jinsi Mama na Watoto walivyokua na Amani Na Kushirikiana Kutoa Neno la Pamoja Kwa Nip

Katika Video Hii Yupo #LaurenLondonAmbae alikua mpenzi wake, Watoto wake #Kameron #Kross Pamoja na #Emani

By Ally Juma.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW