Burudani

Rapper Nipsey Hussle kupewa heshima ya mwisho kwenye ukumbi alioagiwa Michael Jackson

Wengi wakimjua kama Nipsey Hussle lakini jina lake la kuzaliwa likiwa ni Ermias Joseph Asghedom aliyezaliwa miaka 33 iliyopita August 15, 1985 kusini mwa Los Angeles nchini Marekani na kupoteza maisha yake March 31, 2019 (age 33) Los Angeles, California, U.S.A ikiwa ni nje ya duka lake la nguo. ambalo linaitwa ‘The Marathon Clothing”

Baada ya kupoteza maisha Wasanii maarufu nchini Marekani wakiwemo Drake, Rihanna na J Cole wametoa rambi rambi zao kufuatia kifo cha rapa wa Los Angeles Nipsey Hussle, ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi mjini humo. Msanii huyo wa miaka 33 alipigwa risasi nje ya duka lake la kuuza nguo.

Lakini kutokana na msiba huu familia ya marehemu Nipsey Hussle imethibitisha kuwa mwili wa mpendwa wao utaagwa siku ya Alhamis April 11,2019 katika ukumbi wa Staples Center uliopo mjini Los Angeles Marekani. sehemu amako alipigiwa risasi na ndio yalikuwa makazi yake hata duka ambalo alikuwemo kabla ya mauti kumfika lipo Los Angeles.

Inaelezwa kuwa ukumbi huo una uwezo wa kubeba jumla ya watu 21,000 na shughuli za kuuga mwili huo zitaanza mapema asubuhi huku taarifa nyingine zikiripoti kuwa tiketi zimeanza kuuzwa mtandaoni kwa ajili ya watu kuingia eneo hilo na wamiliki wa tiketi pekee ndio watapata nafasi ya kuingia.

Ikumbukwe Ukumbi huo ulitumika kuuaga mwili wa mfalme wa Pop duniani Marehemu Michael Jackson mwaka 2009.

By Ally JUma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents