Habari

Rapper P. Diddy amtakia ‘Happy birthday’ Nelson Mandela

Leo (July 18) muasisi wa taifa la Afrika Kusini Nelson Rolihlahla Mandela anasheherekea siku yake ya kuzaliwa kwa kufikisha miaka 95 huku afya yake ikiwa bado inaendelea kuimarika taratibu akiwa bado hospitali. Ukubwa na umaarufu wa Mandela sio tu kwa taifa lake na Afrika pekee kwani hata wanamuziki maarufu kutoka Marekani kama Diddy wanatambua mchango wake katika mengi aliyoyafanya hapa duniani.

mandela2

Rapper na mmiliki wa kituo kipya cha TV ‘Revolt’ Sean Combs aka P.Diddy amemu wish Madiba ‘happy birthday’ kupitia akaunti yake ya Instagram na kuweka picha yake pamoja na maneno haya “Happy Birthday Mr. Mandela!!!! Thank you for all you have done!!”

diddy

Nelson Mandela alizaliwa tarehe 18 Julai, mwaka 1918 na ndiye Rais wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia nchini Afrika Kusini. Alikuwa mwanasheria na mwanachama wa ANC aliyepinga siasa ya ubaguzi wa rangi ‘Apartheid’ nchini humo. Madiba alitumikia kifungo cha miaka 27 kutokana na harakati zake za kuupinga ubaguzi wa rangi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents