Burudani

Rapper Rich Homie atiwa mbaroni na polisi

Rapper wa Marekani, Rich Homie Quan amekamatwa na polisi wa mjini Atlanta baada ya kukutwa na bunduki pamoja na madawa ya kulevya.

Quon ambaye anafanya kazi na lebo ya kujitegemea ya T.I.G. Entertainment alikamatwa na polisi hao wakati akitoka katika show yake ya muziki siku ya Jumamosi ya Mei 28 katika klabu ya Liquids iliyopo Wadley.

Polisi hao walimtaka Quan na wenzake watano wasachiwe ndipo wakakutwa na silaha pamoja na madawa ya kulevya aina ya bangi ambayo ni kinyume na sheria. Siku ya Jumapili rapper huyo alipelekwa katika jela ya Jefferson County huku uchunguzi ukiwa unaendelea.

Tukio hilo linaweza kuchelewesha kutoka kwa albamu yake ‘Rich as in Spirit’ ambapo Lil Wayne, Ashanti, Jadakiss, na Boosie Badazz wanatarajiwa kusikika ndani yake.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents