Moto Hauzimwi
Shinda na SIM Account

Rapper wa Kenya Femi One aeleza sababu ya kuwashirikisha wasanii wengi kwenye remix yake

Rapper Femi One kutoka nchini Kenya, amefunguka kuhusu wasanii abao amewashhirikisha katika wimbo wake mpya ‘Tippy Toe Remix’.

Katika wimbo huo rapper huyo wa kike ambaye yupo chini ya lebo ya Kaka Empire, amewashirikisha baadhi ya wasanii wengine ambao wapo katika lebo hiyo akiwemo King Kaka,Kristoff, Fena Gitu, Timmy Tdat na DJ JR.

Akiongea na Bongo5, msanii huyo amesema, “Nimefarijika sana kwa kufanya kazi na wasanii hawa wakubwa kwenye remix hii.”

“Nimejifunza mengi kutoka kwewnye kazi zao. Ninajivunia kwa Fena Gitu na Timmy Tdat ambao wamependekezwa. Kristoff ni genius kwa kuusikia muziki mzuri na uwezo wa King Kaka wa kukaa kwenye muziki wowote ni mkubwa,” ameongeza.

Leave a comment

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW