Burudani

Rapper Wale ametangaza nafasi ya kazi kwa mashabiki wake wanaotafuta ajira

Rapper Wale kutoka Marekani ametangaza habari njema kwa mashabiki wake na wapenzi wa muziki ambao wamesomea au wana ujuzi na fani ya U-DJ.

Image result for wale
Wale

Wale kupitia ukurasa wake wa Twitter aliweka tangazo hilo kwa ku-tweet “Nahitaji DJ mmoja ..nina uhitaji wa haraka” Tweet ambayo muda mfupi baadae aliifuta.

Hata hivyo, alipoulizwa na mdau mmoja mtandaoni kuwa ni DJ gani anayemuhitaji, Wale alisema kuwa yeyote yule awe wa Studio au wa kwenye matamasha.

Tayari watu zaidi ya elfu moja wameshatuma maombi yao kupitia ukurasa wa Twitter na pengine huenda ikawa ndio sababu ya Wale kufuta Tweet hiyo, ila bado usikate tamaa na wewe unaweza ukarekodi kipande chako cha video au audio na kisha um-tag Wale kwenye mitandao ya kijamii.

Hii sio mara ya kwanza Wale kufanya hivyo, kwani mwaka 2015 na 2016 alitangaza nafasi hiyo ya kazi na aliajiri Ma-DJ wawili na amekuwa akifanya hivyo anapokaribia kutangaza ziara yake ya muziki.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents