Burudani ya Michezo Live

Rappers 10 wa Tanzania wanaochukuliwa poa kwa sasa (10 Most Underrated rappers)

Kuna rappers wanaoweza na wanashine pia wapo wanaoweza lakini hubaki tu kawaida – the underdogs. Kuna rappers kibao wenye vipaji, wapya na wa zamani ambao hawapewi heshima wanayostahili, rappers wanaochukuliwa poa. Hii ni orodha ya rappers 10 wakali wa Tanzania wanaochukuliwa poa, 10 most underrated rappers.

1. Jay Mo

http://www.youtube.com/watch?v=JcvEkCL6Py4

Ita rapper yeyote mkali aliyejulikana katika kipindi cha miaka mitano iliyopita muulize ni wasanii gani aliokuwa akiwasikiliza zamani na wakamshawishi, atataja wote lakini hawezi kuacha kulitaja jina la Juma Mchopanga aka Jay Mo. Jay Mo ni rapper mwenye ‘international quality’.

Hakuna anayebisha kuwa Jay Mo ni kati ya wasanii wachache Tanzania wenye hits zaidi ya 10 kali za muda wote (best songs of all time). Kutaja chache tu ni pamoja na Bishoo, Mvua na Jua, Maisha ya Boarding, Kama Unataka Demu, Kimya Kimya, Stori Tatu Tofauti, Money, Famous na zingine.

Rapper huyu mwenye uandishi na style yake mwenyewe aka Mo Techniques Mo Skills, Superman, Mo Genius ni dhahabu ambayo kwa sasa inakanyagwa mchangani. Ni lini mara ya mwisho umesikia jina la Jay Mo limetajwa kuwa atapiga show sehemu?

Si jambo la kushangaza kuona hata nusu ya maoni ya wasomaji wetu waliyotoa kupitia Facebook, yamemtaja Juma kama msanii tight wa kwanza anayechukuliwa poa kwa sasa.

Hata hivyo P-Funk na One the Incredible hawaamini kama Jay Mo ni underrated.

“Jay Mo mimi sihisi kama yuko underrated,” anasema One. Jay Mo tayari ni legend ni msanii anayeweza kwenda na akarudi kama anavyotaka yeye. Unajua kwenye muziki kuna level fulani unafikia hata kama watu wakisema hawakukumbuki lakini comeback yako ipo tu yaani hakutakuwa na mtu mwingine kama wewe.”

“Ambao ni underrated sana ni wale ambao wakitoa ngoma haisikiki kabisa lakini unajua ni mkali,” anasema Majani.

“In some point Jay Mo is underrated but not kivile inavyokuzwa na watu. Because if you have a hit and you go up to number one kwenye top ten you are not underrated anymore isn’t it? Labda useme akina Nikki Mbishi wale ndio the more underrated I guess.”

2. Nikki Mbishi

Nikki Mbishi ni miongoni mwa wasanii wachache wa hip hop wanaoheshimika zaidi na wasanii wengine. Ana uwezo wa hali ya juu wa freestyle, uandishi na kuhimili jukwaa. Uwezo wake wa kukariri nyimbo za wasanii wengine ulimpelekea Profesa Jay amempe aka, Terabyte. Nikki anakubali kuwa watu wanamchukulia poa:

“Me I think I am the most underrated. Mara nyingi mimi vitu vyangu vinakuwa anticipated. Unajua unapokuwa mtu unakaa kimya muda mrefu lakini still people are talking about you, wanauliza uko wapi, unafanya nini, lini unatoa ngoma mpya, watu wanataka kukusikia, kusikia kwenye interview utaongea nini. Kitu nachokijua mimi ni kwamba there is no shining in the underground cause it’s dark in there. All in all when it comes to music they know what I do.” Msikilize zaidi hapa:

3. One

Uwezo wa Moko wa Miujiza ulianza kutambulika kwenye wimbo wa Nikki Mbishi, Kila Siku. Ngoma hiyo ilitoka kipindi ambacho tayari jina la Nikki lilikuwa limeshika. Verse ya One kwenye Kila Siku ilimvutia kila shabiki wa Hip Hop ya Tanzania aliyetaka kumjua zaidi One.

One alikuja kuonesha uwezo wake mwenyewe kwenye ngoma iliyotengenezwa na Duke, One the Incredible. Katika ngoma hiyo One alithibitisha kuwa mfalme mwingine wa uandishi matata wa mashairi ya hip hop amevaa crown.
Katika mtandao wa TZHiphop, Fid Q alimjumuisha One miongoni mwa wasanii watano wa hip hop Tanzania anaowakubali zaidi. Alisema anapenda jinsi anavyotumia Kiswahili fasaha na ule uandishi wake wa kugushi kushoto kisha anaelekea kulia. Uandishi kama huo kitaalamu alisema unaitwa ‘Unorthodox literary’…
Kuhusu kama anahisi yuko underrated, One anasema:

“Kwenye hip hop sifeel kama niko underrated, lakini unapoongelea kwenye muziki wa mainstream, yeah naweza kusema nipo underrated, watu wanaoverlook wanajua ninafanya nini lakini hawafuatilii ni nini kinafanywa.
Watu wanapaswa waelewe kuwa mainstream ni system ambayo imepangwa na watu so kuna certain channels ambazo haziwezi kudeal na wewe kama wewe hauko tayari kudeal nao kwa mapenzi yao. Haiwezekani tu mtu akatoa video yake akafika mpaka namba moja, akachukua tuzo, it’s not usually votes za watu ni vote ya watu fulani ambao wanashawishi watu wengi. Sio kweli kwamba mainstream ni system ambayo ipo kwamba msanii yeyote anaweza akaingia.”

Uandishi na mituo ya One umewaambukiza wasanii wengi wapya walioanza kujulikana baada yake. One ni msomi, anayeweza kuandika maishairi kwa Kiswahili na Kiingereza kwa ufasaha. Ana uwezo wa ajabu apandapo kwenye stage, lakini ni lini umewahi kusikia One ametajwa kuperform kwenye show za mainstream zaidi ya zile za Kilinge cha Msasani Club?

4. Nash MC

Ukikutana na Maalim Nash, ni ngumu kumdhania kuwa ni miongoni mwa wachanaji wenye uwezo usiokamatika. Mzuzu wake mrefu na uvaaji wa suruali ‘njiwa’ humfanya aonekane kama ustaadhi aliyeingiwa na dini ya kiislamu haswaaa na ndio maana anajiita Maalim Nash.

Nach MC anaifahamu Hip Hop vyema. Kama umewahi kuhudhuria Kilinge cha Msasani Club na ukasikia hotuba zake kuhusu hip hop, bila shaka ulimpa salute. Ni muandishi wa mashairi aliyemfuatilia sana Shaaban Robert na ndio maana alitoa mixtape iitwayo Mzimu wa Shaaban Robert.

5. Mapacha

K na D wa Mapacha aka Maujanja Saplayaz, wanajulikana sana kwa kuwa mstari wa mbele kwenye movement iliyokwisha ya Anti-Virus. Pamoja na kutoa nyimbo kali, ni wachache waliouchukulia serious uwezo wao kiasi cha kulazimika kuingia kwenye movement hiyo. Kwa sasa Mapacha ni kama wameukatia tamaa muziki na hivyo kuendelea na shughuli zingine za kutafuta maisha mitaa ya Mwenge, jijini Dar es Salaam.

6. Stopper Rhymez

http://www.youtube.com/watch?v=iD6KJwW7Boo

Stopper ni rapper kutoka Arusha ambaye anafahamika kwa style ya kurap haraka. Pamoja na kufanya hip hop, Stopa ni fundi umeme aliyesomea. Ana style nyingi za kurap kuliko msanii mwingine yeyote. Hilo alilithibitisha kwenye track yake, Style Tatu. Ana uwezo wa kufanya dancehall na ukamsahau. Bahati mbaya ni kuwa hapati heshima anayostahili.

7. Salu T

May 1, 2011 mtandao wa TZHiphop uliandika: Kama wewe ni kijana wa miaka ya 2000 na kuendelea basi bila shaka humfahamu Salu T vizuri. Sio kosa lako; ni siasa tu za hili gemu na vyombo vya habari. Salu T ni mmoja tu ya watu wengi wanaoijua Hip Hop — na wenye vipaji — ambao iliwabidi au imewabidi kuachana na muziki na kuendelea na mambo mengine kwenye maisha yao.

Kutokana na kuchukuliwa poa kwenye muziki, Salu aliamua kwenda kujichimbia Kyela, Mbeya.

“Hakuna mtu aliyerecognize ile potential yangu, nguvu yangu mimi kwenye game, watu hawajaiona bado lakini nimefanya kazi nyingi sana, nimeandika mashairi mengi sana,” alisema Salu T kwenye interview moja.

8. Azma Mponda

http://www.youtube.com/watch?v=knY4fwTFu30

Hivi ndivyo mtangazaji wa kituo cha radio cha Victoria FM, Josefly anamzungumzia Azma:

Inawezekana kabisa jina ‘AZMA’ sio jina linalofahamika kwa watu wengi kama majina ya mastaa wengine, lakini naweza kusema kwa uandishi wa mashairi na idea za kipekee ‘ni dhahabu mchangani sema tu hajashtukiwa’.
Jina lake halisi ni Azma Mponda, Kwa wale wanaoufatilia muziki wa Tanzania bila kujali majina makubwa watakuwa wameshawahi kumsikia kupitia media mbalimbali pamoja na mitandao ya kijamii ama blogs. Alishasikika akionesha uwezo wake mkubwa kwa kufanya mitindo huru katika kipindi cha Kiss Collabo cha Kiss FM, So So Fresh cha Clouds FM, na kuonekana katika Fid Friday Freestyle ya Channel 5.

Azma alishawahi kufanya nyimbo nyingi za Hip Hop zikiwa na ujumbe mbalimbali, lakini ndiye msanii wa kwanza wa Hip Hop Tanzania kufanya mixtape ama album yenye nyimbo 18 na zote zina ujumbe wa mapenzi.

Mfano, Wimbo wake wa ‘Kipimo cha Penzi’ ambao uko kwenye album yake ya ‘Love Stories’ ni wimbo ambao ukiusikiliza lazima utapata kitu kikubwa cha kujifunza, lakini pia ni wimbo mkubwa ambao utakufanya ufikiriea mara mbilimbili mashairi yake, kwa ufupi utakushtua japo ulishawahi kusikia nyingi za mapenzi.

Hiki ndicho kilichomtokea Mwimbaji maarufu Belle 9, ambae alishindwa kuzuia hisia zake alipousikia ‘Kipimo cha Penzi’ hakusita kueleza ukweli wake japo hamfahamu Azma. Aliandika katika ukurasa wake wa facebook, lakini nilipomtafuta na kupiga nae story haya ndiyo aliyosema.

“Hii ngoma ya Azma imenishawishi mimi kwa kiwango kikubwa sana kwa sababu nilikuwa sijapata nafasi ya kuusikiliza lakini nilivyosikiliza nilivyogundua kitu alichoimba, umekuwa ni wimbo wa pili kunishangaza kwa sababu wimbo wa kwanza kunishangaza wa mapenzi toka nimeanza kuzisikilza nyimbo za mapenzi ni wimbo wangu wa ‘sumu ya penzi’, ni wimbo ambao niliandika mwenyewe lakini nashindwa kuuzoea na unanishangaza mpaka leo, lakini sijawahi kushangazwa na wimbo mwingine wa mapenzi, wimbo wa Azma ni wimbo mkubwa sana, ameongea vitu deep, mpaka ikafikia kipindi nikatafuta namba yake nikampongeza kwa kitu ambacho amekifanya, ni ngoma kubwa sana yaani.”

Changamoto ni kwamba dhahabu zilizo mchangani kama Azma ni nyingi lakini kuna ugumu sana katika kupiga hatua kuonekana kutokana na mfumo mzima wa soko la muziki kibongobongo, anauza tape mkononi, na pia changamoto ya promotion ni kubwa sana kwake.

9. Gosby

Gosby ana style, anaandika and he got the swag na ndio kitu kilichomvutia Hermy B kufanya naye mikono kadhaa. Ni rapper mwenye international quality; kitu ambacho kimewafanya watu wanaoujua muziki juu juu wasikitambue kipaji chake.

10. Wakazi

Wakazi a.k.a Swagga Bovu aliyezaliwa kwa jina la Webiro Noel Wassira anachukuliwa poa kwasababu tu nyimbo zake hazipati airtime ya kutosha redioni.

Hivi karibuni alikuja Tanzania baada ya kukaa kwa muda mrefu nchini Marekani. Alifanikiwa kukutana na wasanii kibao hasa kwenye maeneo panapofanyika shows na kuonesha uwezo wake. Kwa wale ambao waliweza kumshuhudia kwenye Kilinge, walifanikiwa kukiona kipaji chake kilivyo mbali. Tatizo ni kuwa redio nyingi za kibongo bado hazijamuelewa pengine ni kutokana na kutumia muda mwingi akiwa Marekani.

Kitu ambacho watu wengi hawakifahamu ni kuwa Wakazi anakubalika mno hata na wasanii wakubwa wan chi zingine na ndio maana msanii mkubwa wa Ghana aitwaye Reezon alimshirikisha kwenye ngoma yake, Weekend.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW