Habari

Rashid Matumla mchovuuu kwa Maneno Oswald


Kama ulitazama mahojiano ya weekend iliyopita kupitia kituo cha runinga cha TBC1 yaliyowahusisha mabondia wawili wakongwe nchini, Maneno Oswald aka ‘Mtambo wa Gongo’ na Rashid Matumla aka ‘Snake Boy’ bila shaka ulijionea burudani nzuri.

Yalitawaliwa na tambo nzito baina yao kiasi cha kuanza kusogeleana na kunyoosheana mikono hadi mtangazaji aliyekuwa akiwahoji kuwakatisha kwa muda kwakuwa huenda wangezichapa hapo hapo studio na kuzua mambo mengine.
Kila mmoja alitamba kuwa angeshinda.
Hata hivyo ukweli ulijulikana juzi siku ya Eid Mosi pale katika viwanja vya Dar Live ambapo Maneno Oswald alimtandika vilivyo Rashid Matumla.
Katika pambano hilo la kwanza kati ya mapambano matatu waliyojiwekea mabondia hao ambapo kama mmojawapo akishindwa yote atalazimika kustaafu ndondi, Rashid Matumla alionesha wazi kuwa ameshakuwa mchovu.
Mtambo wa Gongo alitawala raundi nyingi kati ya 10 walizokuwa wanapigana kiasi cha kumlegeza Matumla ambaye almanusra aende chini kama gunia.
Majaji Pembe Ndava, Agapeter Mnazareth na Rajab Mlowe walitoa pointi 97-93, 96-94 na 97-93 na kumpa ushindi Oswald.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents