Burudani

Rasmi: Alikiba kuoa usiku wa leo, Mama Mkwe anena

By  | 

Msanii wa muziki Bongo, Alikiba anatarajia kuoa usiku wa leo.

Kwa muijibu wa Pilipili FM, Alikiba anafunga ndoa na mpenzi wake, Aminah Rikesh, Mombasa nchini Kenya.

Mama wa Bibi Harusi amesema; “Tunasherekea harusi ya mtoto wangu anaolewa na Alikiba, tunashukuru Mwenyenzi Mungu atupe furaha, anayepanga ni yeye hakuna anayeweza kupangua hata kama Alikiba ametoka TZ lakini Mungu ndiye ameshapanga”.

Soma Pia; Mahusiano ya Alikiba na mrembo wa Kenya yaanza kuvuja

Licha ya wawili hao kufanya siri mahusiano yao hadi kufikia hatua ya kuoana, taarifa za ndani zinadai kuwa Alikiba na Aminah wameanza kuwa pamoja tangu mwaka 2016

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments