Burudani ya Michezo Live

Rasmi Cristiano Ronaldo ajiunga na Juventus ya Italia

Klabu ya Real Madrid imethibitisha mshambuliaji wake, Cristiano Ronaldo amejiunga na Juventus ya nchini Italia.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotoka hivi punde klabu hizo mbili zimeafikiana malipo ya pauni milioni 105 kwaajili ya nahodha huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 33.

Ronaldo ambaye ni mshindi mara tano wa Ballon d’Or ametumia misimu tisa Madrid baada ya uhamisho wake wa pauni milioni 80 akitokea Manchester United huku akiondoka na kuwacha rekodi ndani ya klabu hiyo kwa kufunga jumla ya mabao 451.

Nahodha huyo wa Ureno anaondoka Real baada ya kushinda mataji mawili ya La Liga titles, mawili Copa del Rey na mataji manne ya klabu bingwa barani Ulaya.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW