Aisee DSTV!

RASMI: Huawei wazindua mfumo wao endeshi mpya wa ‘Harmony-OS’, Waahidi kuwapoteza Android sokoni

Hatimaye kampuni ya Huawei imezindua rasmi mfumo wake endeshi (Operating System) ujulikanao kwa jina la Harmony-OS utakaotumika kwenye simu zao za Huawei.

Mfumo huo umezinduliwa leo Agosti 9, 2019 kwenye mkutano wa wabunifu wa kampuni hiyo nchini China, ikiwa ni mizezi michache imepita tangu Kampuni hiyo ifutiwe kibali cha kutumia mfumo endeshi wa Android.

Akiongea kwenye mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Richard Yu amesema kuwa mfumo huo utakuwa wa spidi zaidi kwenye simu na Smart TV kuliko hata ule wa Android.

Yu amesema kuwa mfumo wa HarmonyOS ulianza kutengenezwa mwaka 2017 ulijulikana kwa jina la HongmengOS kabla ya leo kuzinduliwa.

Mfumo wa HarmonyOS utaanza kutumika rasmi kwenye matoleo mapya ya Honor Series na kwa watumiaji wa simu za zamani zenye mfumo wa Android watachagua aidha waendelee kutumia Android au kubadilisha mfumo wa HarmonyOS.

Kiutendaji, mfumo huo utasapoti program zote zilizoandikwa kwa kutumia lugha ya kompyuta ya HTML5 pamoja na Linux.

Kwenye mkutano huo pia, Huawei wamesema kuwa lengo la mfumo wao mpya wa HarmonyOS ni kupindua soko la mfumo wa Android duniani, Huku wakiaminisha umma kuwa mfumo wao ni bora na ni salama zaidi.

Chanzo: https://luram.co.ke/newsbyte/2019/08/09/harmony-os-huaweis-answer-to-the-android-ban/

 

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW